HECTOR BELLERIN AWACHOMOLEA BARCELONA MCHANA KWEUPEE

INAKUWAJE hii. Klabu inafanya mazungumzo ya siri na mchezaji wa timu nyingine mnafikia makubaliano lakini baadaye mchezaji huyo anakuwa nunda mkipiga simu anakata.

Hiki ndicho kituko ambacho amefanya beki wa Arsenal, Hecter Bellerin ambaye amesema kwamba matajiri wa Hispania, klabu ya FC Barcelona walikuwa wamsajili lakini baadaye ameona ili kuepuka usumbufu awakatie simu zao.

Bellerin amesema kwamba ni kweli alikuwa anataka kusajiliwa na Barcelona lakini baadaye akagundua kwamba kuna haja ya kulinda kipaji na heshima yake anayoipata katika Arsenal.

“Wakati mwingine si tabia njema kabisa lakini unaona kwamba ni kama umeshachokoza mambo na sasa unatakiwa kuyaepuka. Nilikuwa nirejee Hispania kucheza katika nchi yangu lakini heshima ninayopata hapa ni kubwa zaidi,” amesema.

Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alikaa kwa miaka minne katika klabu hiyo ya Barcelona kabla Arsenal hawajamnyakua mwaka 2011 na sasa Barca wanataka kumrejesha nyumbani.

Kocha Arsene Wenger alikuwa akimtumia Bellerin kama nyota kiraka na katika msimu wa 2014/15 alikuwa chaguo lake namba moja baada ya kuumia kwa Mathieu Debuchy na Calum Chambers.

“Nimekuwa nikisumbuliwa pia mpaka na baadhi ya ndugu zangu wakinitaka nirejee Nou Camp lakini pi nimewapa msimamo kwamba natakiwa kulinda kipaji na heshima yangu."

"Ndio kwanza nina miaka 21 unadhani nimechoka kucheza nje ya Hispania. Hapana natakiwa kurejea huko nikiwa nimeshatimiza malengo yangu,” amesem Bellerin.


Akihojoiwa na Deutche Welle TV kama iktokea kwamba astaendelea kupata usumbufu kutoka Barcelona, amesema kwa kifupi tu “Hata simu zao soitazipokea kabisa.”

No comments