STAA Beyonce amewashangaza mashabiki baada ya kujigundua annatokwa na damu sikioni lakini akaendelea kupagawisha jukwaani.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa tamasha la Tidal X lililofanyika Jumamosi usiku jijini New York City, baada ya heleni ya mwanamama huyo kupasuka na kumchana sikio wakati akitumbuiza kwenye ukumbi wa Brookly’s Barclays Center.

Akiwa anatumbuiza kibao chake kiitwacho Ghost Haunted, Beyonce aliijishika eneo alipoumia na kisha akajipangusa damu kwa vidole na huku akiendelea kuimba.


Kutokana na tukio hilo baadhi ya mashabiki walituma kwenye mitandao ya Twitter picha za video zikimuonyesha Bayonce akiangalia sikio lake likivuja damu na huku akiendelea kuimba.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac