HUU NDIO WIMBO WA LEYLA RASHIDI UNAOMVUTIA ISHA MASHAUZI

RAIS wa Mashauzi Classic Modern Taarab, Isha Mashauzi ameshindwa kuficha hisia zake pale alipoamua kuweka wazi kuwa akipenda zaidi kibao cha mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Leyla Rashid, “Maneno ya Mkosaji”.

Katika kuthibitisha hilo aliloliongea ndani ya Studio za Radio Free Afrika, katika kipindi cha “Kona ya Mwambao”, Isha aliiimba kwa ufasaha sehemu ya kibao hicho kilichomo kwenye albamu ya kwanza ya Jahazi Modern Taarab, “Two In One”.
Leo hii baadae, Leyla na Isha watakutana uso kwa uso, kwenye pambano kali lililoandaliwa maalum kwa ajili yao, ndani ya Darlive, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam ambapo kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

No comments