Habari

INIESTA AFICHUA SIRI YAKE NA KOCHA PEP GUARDIOLA

on

NAHODHA na kiungo wa mabingwa
wa soka nchini Hispania FC Barcelona, Andres Iniesta amefichua siri iliyokuwa
ikiendelea kati yake na meneja wa sasa wa Manchester City, Pep Guaridiola wakati
wa usajili wa majira ya kiangazi.
Iniesta amesema Guaridiola
alionyesha nia ya kutaka kumsajili na kumpeleka Etihad Stadium lakini alikataa
wito huo kwa kuamini England hapakuwa mahala sahihi kwa soka lake.
Iniesta ambaye alikuwa sehemu
ya kikosi cha Barcelona wakati Guardiola akiliongoza benchi la ufundi la
klabu hiyo kati ya mwaka 2008-2012, amesema lengo lake kubwa kwa sasa ni kutaka
kumalizia soka lake akiwa Camp Nou.
Hata hivyo amedai kuwa
anamuheshimu sana Guaridiola na bado ataendelea kuwa mtu wake wa karibu hivyo
amevitahadharisha vyombo vya habari kutolichukua suala la kukataa kwake kwenda Man
City kama kuna ugomvi baina yao.
Kiungo huyo mwenye umri wa
miaka 32, kwa sasa ni mchezaji mkongwe katika kikosi cha FC Barcelona baada ya
kuondoka Carlos Puyol pamoja na Xavi Hernandez ambao kwa pamoja walicheza
michezo 505 wakiwa Camp Nou.

Iniesta ameshacheza michezo
392 akiwa na FC Barcelona na amebahatika kufunga mabao 34 tangu mwaka 2002
alipopandishwa kutoka kikosi pili hadi kikosi cha kwanza.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *