ISCO AFUNGUKA NA KUSEMA HANA MPANGO WA KUSEPA REAL MADRID

ISCO ni kama amepasua jipu lililokuwa linasubiliwa kutumbuka baada ya kuthibitisha kuwa hana mpango wa kuihama Real Madrid licha ya kuwapo kwa tetesi zinazomhusu.

Hatua ya Isco kuweka hadharani msimamo huu unafuatia umuvi uliopo sasa unaomtaja kutaka kuachana na kikosi hicho cha Santiago Bernabeu.

Alihusishwa na tetesi za kutaka kutua katika kikosi cha Wekundu wa jiji la Manchester United ingawa pia alihusishwa na kutaka kutua Stamford Bridge.

Mnamo mwezi Agosti mwaka huu alivumisha pia kutaka kusajiliwa na Tottenham Hotspur lakini hata hivyo dilililishindikana.

Akakanusha Isco alisema: “Ninahusishwa kuondoka hapa lakini ni jambo lisilo na ukweli.”

“Sikweli kwani nina miaka miwili ya mimi kubaki hapa ndani ya Santiago Bernabeu."

“Ingawa bado hakuna mazungumzo juu ya kandarasi yangu lakini ninachoamini bado nitaenderea kuwa hapa.”

“Sijajua nini kitatokea baadae lakini kuwa na msimamo ni jambo la mahana la maana na umuhimu pia” alisema Isco.


Pamoja na Tottenham pia Isco anatajwa katika uvumi wa kutua Old Trafford chini ya kocha Jose Mourinho.

No comments