Habari

ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUKATA MZIZI WA FITNA LEO USIKU DAR LIVE

on

HATIMAYE waimbaji wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi
sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali leo Oktoba 22 ndani ya
ukumbi Dar Live Mbagala.
Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi
atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka
kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.
Bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic
zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.
Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa baada
ya majigambo mengi kutoka kila pande, leo mzizi wa fitna utakatwa ndani ya Dar
Live.
Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali
kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo
kamwe Isha hawezi kuyagoka.
Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa
Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *