ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUPAMBANA OKTOBA 22 …Jahazi na Mashauzi Classic kusindikiza …ni Nani Zaidi ndani ya Dar Live


WAIMBAJI wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala.

Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.

Mratibu wa onyesho hilo Hajji Mabovu amesema bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.

Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa wamefikia makubaliano ya kuonyeshana ubabe Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu.

Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka.

Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.

No comments