WAIMBAJI wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid ambao watapambana vikali Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala, wamechafua hali hewa.

Siku chache baada ya taarifa za mpambano huo kuwekwa hadharani, mashabiki wa pande zote mbili wameingia kwenye vita vikali kupitia mitandao ya kijamii.

Mashabiki hao wamekuwa wakitupiana maneno makali na wakati mwingine hata kutukanana, hali inayoonyesha kuwa onyesho hilo litakuwa ni la vuta ni kuvute.

Bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac