JAHAZI MODERN TAARAB YAUNGURUMA LUNCH TIME NA KUSUUZA NYOYO ZA MASHABIKI

JAHAZI Modern Taarab Jumapili ya jana walitimua vumbi la haja ndani ya kiwanja cha Lunch Time, Manzese Tiptop, jijini Dar es Salaam na kumudu vilivyo kukonga nyoyo za mashabiki wao.

Muziki safi uliokusanya sauti za waimbai wao mahiri pamoja na ala zilizokuwa zikikung’utwa na wasanii wao nguli, vilikuwa chachu kubwa ya kuwafanya mashabiki kuacha viti vyao na kujaa kati kujimwaga kwa raha zao.


Picha saba zifuatazo hapo chini zinaeleza namna mambo yalivyokuwa ukumbini ambapo ilikuwa hapatoshi na kila aliyehudhuria aliondoka akiwa kasuuzika na roho yake.
 Mwimbaji Mariam Mwinjuma akipagawisha mashabiki
 Prince Aboubakar Soud "Amigo" nae akiwajibika 
 Mwimbaji chipukizi Mish Mohammed akifanya yake
 Rahma machupa akikinukisha
 Fatma Kassim akiwakoleza mashabiki wao kwa songi lake jipya la "Kamwe Siumbuki"
 Mkongwe Khadija Yussuf "Sauti ya Chiriku" kama kawaida yake hakutaka kukosea
Hapa mzuka umewapanda mashabiki na kuamua kujimwaga katikati kuchizika

No comments