JAY Z AELEKEZA NGUVU KWENYE BIASHARA, UANDAAJI VIPINDI RUNINGANI

MKALI wa Hiphop, Jay Z ameendelea kujiongezea fursa za kujikusanyia fedha na anadhihirisha licha ya kuwa na utajiri mkubwa kutokana na muziki, bado ana vitu vingi ambavyo bado hajavikamilisha.

Na sasa anaelekeza nguvu zake kwenye uandaaji wa vipindi vya Televisheni na filamu ambapo mjasiriamali huyo ametia saini mkataba wa miaka miwili na kampuni inayojihusisha na masuala hayo ijulikanayo kama “Western Company” ambapo Jay Z atasaidia zaidi kuendesha uandaaji wa filamu za vipindi vya Tv.


Jay Z ambaye jina lake halisi ni “Shawn Carter”, tayari anasifika kwa kuwa na kiwanda kikubwa cha utayarishaji, zikiwemo lebo zake za “Roc-A-Fella”, “Def Jam” na “Roc Nation” lakini anaonekana wazi kutaka kujiendeleza zaidi kwenye tasnia hii ya burudani kwa kujihusisha na utayarishaji tofauti wa vipindi vya Tv na filamu.

No comments