JE UNAJUA? GUARDIOLA HAJAKOMA KUMPA AGUERO PENATI!

LICHA ya kukosa mkwaju wa penati katika mchezo wa Jumatatu dhidi ya Everton, staa wa Manchester City, Sergio Aguero ataendelea na jukumu hilo.

Kauli hiyo imetolewa na kocha wa kikosi hicho Pep Guardiola ambaye amedaikuwa hatosita kumpa penati straika huyo wa kimataifa wa Argentina.

“Napenda wachezaji wenye sifa za kupiga penati. Napenda hilo, sitosema jukumu lakumu la kupiga penati ni la mtu mmoja,” alisema Guardiola.

Ikumbukwe kuwa Aguero alikosa penati mbili katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Steaua Bucharest.

No comments