JENGUA ATANGAZA KUCHEZA BURE FILAMU ZA WANAOCHIPUKIA ILI KUWASAIDIA KUWAINUA

MSANII wa siku nyingi wa Bongomuvi, Mohammed Fungafunga "Jengua" amesema anaweza kufanya filamu hata bure ili kuwasaidia wasanii wachanga nao waweze kupata mafanikio.

“Nimekuwa nikijitolea kwenye filamu nyingi sana kwa sababu mimi nimekuwa nikishirikiana na hawa wasanii lakini pia ninaamini kwamba wasanii tuko sawa ila sisi tumepata bahati tu yakuonekana hivyo ninashirikiana sana na hawa wasanii wachanga kwa lengo la kuwakuza,” alisema Jengua.

Alisema, hata yeye alikuzwa na wasanii wakongwe enzi hizo kama mzee Kipara, mzee Pwagu na wengine ambao walipata ubunifu bila tatizo hivyo na yeye anapaswa kusaidia wengine.


“Mimi kuna filamu nacheza hata bure ili kuwasaidia hawa wasanii wachanga nao waweze kutoka, huu kwangu ni msaada mkubwa sana kwao na moja ya mikakati ya kuwasaidia wawe juu,” alisema.

No comments