JERMAINE JENAS ASEMA ARSENAL INATISHA ZAIDI GIROUD AKIWEMO KIKOSINI

ARSENAL inatisha zaidi ikiwa na Olivier Giroud kikosini, kwa mujibu wa nyota wa zamani wa England, Jermaine Jenas ambaye sasa ni mchambuzi wa soka.

Straika huyo Mfaransa amepoteza namba katika kikosi cha kwanza msimu huu kufuatia mapumziko marefu baada ya fainal za Euro 2016 na kisha kuumia kidole cha mguuni.

Alifunga mara mbili wakati alipoingia kutokea benchi katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Sunderland juzi.

Na licha ya Arsenal kufurahia ushindi wa mechi nne mfululizo za kuleta upinzani kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England, Jenas anaamini kwamba kikosi cha Wenger kingenufaika zaidi kikiwa na Groud ndani.


“Bado nadhani wanakuwa timu bora zaidi ikiwa Groud kikosini,” kiungo huyo wa zamani wa Tottenham aliiambia BBC Five Live. 

“Ni kwasabasbu tu akiwemo uwanjani anawawezesha vyema Sanchez, Iwobi, Walcot, Ozil wote nyuma yake wacheze vyema zaidi ikiwa mbele.”

No comments