JOHARI ASEMA KUWALETEA MAPOZI MASHABIKI NI KUJIMALIZA KISANII BILA KUJIJUA

MSANII wa filamu Blandina Chagula “Johari” amesema hawezi kuwaletea mapozi mashabiki kwasababu anajua kwamba ndio waliomfanya ajulikane na kupata jina kubwa kwenye Bongomuvi.

“Nasema hivyo kwasababu wasanii wa Bongomuvi tumekuwa tukilalamikiwa sana kwamba tunaringa. Inawezekana kweli wapo wanaoringa lakini hilo kwangu halipo kabisa kwasababu ninatambua mchango wa mashabiki wangu,” alisema.

Alisema kuwa, kwa msanii anayejua anachokifanya hawezi kuringia watu na kujiona yuko juu kuliko wao bila kujua kwamba hao anaowaringia ndio waliomfikisha juu na wanaweza kumshusha.


Huwezi kumjua shabiki kwa jina wala sura, lakini cha msingi ni kwamba unapochangamkiwa na watu hata huwajui elewa kuwa hao ndio mashabiki wako wanaokuweka mjini na hutakiwi kuwaringia,” alisema Johari.

No comments