John Obi Mikel admits he has 'never ran so much' as under new Chelsea coach Antonio Conte

KIUNGO wa Chelsea  John Obi Mikel amefunguka kuwa mfumo wa kocha Antonio Conte wa kufanya mazoezi  mara mbili kwa siku yamewafanya wawe fiti zaidi kuliko ilivyokuwa msimu uliopita chini ya Jose Mourinho.

Mikel amesema walikuwa na mwanzo mbaya msimu uliopita na kulazimika kuangukia nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi.

Chelsea ilifanya vibaya na kuweka rekodi mpya ya mwendo mbovu wa bingwa mtetezi katika Premier League - Mikel anaamini hilo lilichangiwa na wachezaji  kutokuwa fiti pamoja na muda mfupi wa maandalizi ya msimu mpya.

Conte ameleta mageuzi mapya ya mfumo wa mazoezi pamoja na kubadilisha mlo wa wachezaji hali inayomfanya Mikel aamini kuwa Chelsea itaimarika kadri msimu unavyosonga mbele.
The Italian introduced double training sessions to improve players' fitness from last term
Conte amemwagiwa sifa na Mikel
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac