KOCHA Jose Mourinho ni kama bado hajiamini na safu yake ya ulinzi hivyo ameanza kujiuliza nini cha  kufanya kwa ajili ya dirisha dogo la majira ya baridi la mwezi Januari mwakani.

Katika kutambua hilo tayari kocha huyo amewatuma mawakala nchini Ureno kwa ajili ya kufuatilia kiwango cha ulinzi wa timu ya Benfica, Alex Grimaldo.

Alex Grimaldo mwenye umri wa miaka 21, ni mchezaji kijana aliyelelewa katika kikosi cha pili cha timu ya Barcelona ambaye sasa anaingizwa katika kundi la wachezaji wanaowindwa na klabu mbalimbali balani Ulaya.

Jose Mourinho ni kati ya makocha wanaovutiwa na kiwango cha beki huyo ambaye na mtaalamu wa kupiga mipira iliyokufa sambamba na umakini katika kuwadhibiti washambuliaji wenye kasi.

United wameweka mzigo mezani kiasi cha pauni mil 51 kwa ajili ya kukamilisha dili hilo mapema mwezi Januari mwakani wakiamini klabu ya Benfica hawatakuwa na kikwazo cha kumruhusu Grimaldo kutua Old Trafford.


Kwa upandewa Benfika ni kama watajitengenezea faida kwa mlinzi huyo kwani walimnunua kwa pauni mil 1. 25 kutoka Barca, dili lililotimia mnamo mwezi Januari mwaka huu.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac