JOSE MOURINHO "AMWANDAMA" STRAIKA ROMELU LUKAKU

KAMA unadhani kocha Jose Mourinho ameridhishwa na usajili alioufanya hadi kufikia mwishoni mwa msimu huu basi utakuwa umekosea, kwani bado ana mahesabu makali.

Safari hii kocha huyo ameanza kumfukuzia straika wa timu ya Everton, Romelu Lukaku.

Siyo Lukaku pekee bali wanataka kusepa na straika Seamusi Coleman ambao wote wanacheza kama mapacha dimbani.

Lukaku yupo katika kiwango kizuri kwa hivi sasa na Mourinho amemweka katika rada za usajili wa majira ya baridi.

Ukiachana na azma ya Mourinho juu ya Coleman pia mfumania nyavu huyo alikuwa chaguo la kwanza la aliyemtangulia, David Moyes.

Moyes alikuwa anamfuatilia Seamusi Coleman kama aina ya wachezaji ambao aliamini wangeipa mafanikio Manchester United.

Akinukuliwa, Mourinho alimzungumzia Lukaku kama mchezaji anayeweza kuja kuongeza nguvu katika safu ya ushambiliaji.

Kwa sasa Mourinho analazimika kumtumia Antonio Valensia akishirikiana na Matteo Darman.


Katika kiuhakikisha anaweza kumnasa, Mourinho aliwatuma mawakala kufuatilia kiwago cha Lukaku katika mechi iliyowakutanisha Everton dhidi ya Crystal Palace.

Anaamini Lukaku anaweza kucheza sambamba na Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba.

No comments