JOSE MOURINHO AUKINGIA KIFUA UNAHODHA WA ROONEY

UTAMWAMBIA nini kocha Jose Mourinho hadi akuelewe kuhusu nahodha wa kikosi chake cha Manchester United, Wayne Rooney.

Jamaa amewaka sana alipoulizwa kwa nini asimtose na kumpa mchezaji mwingine nafasi hiyo kutokana na mshambuliaji huyo kutocheza kila mara.

Mourinho alisema kuwa Rooney ndie kiongozi wa wachezaji ndani na nje ya uwanja, hivyo kwake yeye lazima aendelee kumheshimu.

Rooney alipata nafasi ya kuanza katika mechi mbili pekee za hivi karibuni dhidi ya Leicester City na ule wa Europe League dhidi ya Zorya Luhansk.

“Kila mahali kuna kiongozi na kwa hapa kwetu Rooney ndie kiongozi kwa sasa, sijui wanaompinga wanamtaka nani na kwa sababu zipi, wachezaji wote wanamkubali kama kiongozi wao,” alisema Mourinho.


Aliongeza kusema kuwa mshambuliaji huyo anachezeshwa katika mechi maalum ikizingatiwa kuwa timu hiyo msimu huu inakabiliwa na mechi nyingi na wamepania kutwaa mataji.

No comments