JOSE MOURINHO KUMLAMBISHA JUAN MATA MKATABA WA MIAKA MINNE MANCHESTER UNITED

IMERIPOTIWA kuwa kiungo wa Manchester United, Juan Mata atapewa mkataba mpya Old Trafford baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Hispania alitarajiwa kuondoka Old Trafford majira ya joto kufuatia ujio wa Jose Mourinho ambaye alimuengua Mata Chelsea na kumuuza United mnamo 2014.

Mata amepewa nafasi ya kung’ara msimu huu baada ya kumzidi kiwango nahodha wa mashetani wekundu, Wayne Rooney katika nafasi yake kama mwanzilishi mkuu wa mashambulizi.

Kwa mujibu wa The Mirror, Mata 28, ambaye mkataba wake unatarajiwa kufika mwisho msimu ujao wa majira ya joto, atasaini sasa mkataba mpya wa miaka minne na miamba hao wa Old Trafford wiki kadhaa zijazo.

Beki Timothy fuso – Mensah pia ni miongoni mwa wachezaji wanatarajiwa kupewa mkataba mpya licha ya kukosa muda wa kutosha kwenye kikosi cha United Ligi Kuu Uingereza msimu huu.

No comments