JOSE MOUROINHO ASHANGAZA WACHEZAJI WAKE MANCHESTER UNITED

JOSE Mourinho amewaamuru wachezaji wa Manchester United wanaoishi kwenye hoteli ya Lowry waende Old Trafford wakaungane na wenzao kisha ndio wapande basi kuja pamoja katika hoteli hiyo kuelekea mechi zao za nyumbani.

Wachezaji wa timu hiyo hukaa pamoja katika hoteli hiyo ya nyota tano iliyopo katikati ya mji kabla ya mechi za uwanja wa nyumbani.

Nyota wa timu hiyo hushushwa ama kuacha magari yao katika uwanja wa klabu hiyo umbali wa kama maili mbili hivi na kuchukuliwa kwa basi la pamoja hadi katika hoteli ya Lowry.

Kocha wa United, Jose Mourinho ana imani za giza na anataka wachezaji wake wakutane wakati aisaka namna ya kumaliza mwendo mbaya wa timu yake.

Siku za nyuma wachezaji kama Paul Pogba, Henrikh Mkhitaryan ambao wanaishi katika hoteli hiyo waliruhusiwa kukutana na wenzao wanapowasili hotelini hapo.

Kanuni hiyo ilitumika pia kwa beki Daley Blind anayeishi katika nyumba ya kupanga, jirani na hoteli hiyo.

Hata hivyo, yote hayo yaliwekwa kando kuelekea mechi ya Manchester derby. Jumatano jioni nyota hao watatu waliamrishwa kuondoka hotelini hapo waende Old Trafford kuungana na wenzao kabla ya muda mfupi baadae kurejea hapo kwa basi la pamoja.


Chanzo kilisema: “Jose ni mtu wa imani ya giza sana.”

No comments