Habari

JUAN MATA AANZA MAZUNGUMZO YA KUSAINI MKATABA MPYA UNITED

on

HATIMAYE kiungo kutoka nchini
Hispania, Juan Mata ameanza kupata mwangaza wa maisha yak echini ya utawala wa
meneja wa Manchester United, Jose Mourinho kufuatia hatua ya kuwa katika
mazungumzo ya kusaini mkataba mpya.
Mata ambaye alikuwa sehemu ya kikosi
cha Hispania kilichotwaa ubingwa wa Dunia wakati wa fainali za Kombe la Dunia
mwaka 2010 ameonyesha kuwa tayari kubaki Old Trafford na kucheza soka la
ushindani kwa vitendo.
Kiungo huyo mwenye miaka 28,
kwa sasa bado ana mkataba wa miaka miwili ambao unamwezesha kulipwa mshahara wa
pauni 130,000 kwa juma, na kama mambo yatakwenda vyema kiasi hicho cha fedha
kitaongezeka.
Mata ambaye aliwahi kucheza
soka akiwa na klabu ya Valencia kabla ya kuelekea nchini Uingereza kujiunga na
Chelsea na kisha Man United, alionekana kuwa adui mkubwa wa Jose Mourinho na
ujio wa Meneja huyo ulitazamwa kwa jicho la tatu kwa kuamini huenda ulikuwa
mwisho wa kiungo huyo.
Mourinho amethibitisha
kuendelea kwamazungumzo baina ya Man United dhidi ya mchezaji huyo na wakati
wowote mambo huenda yakawa sawa.
“Kuna mazungumzo yanaendelea
kati yake na uongozi na nina matarajio makubwa ya kuona jambo hilo
likifanikiwa.”

“Ameonyesha nia ya dhati ya
kutaka kubaki hapa kwa vitendo kutokana na kutumia nafasi ya kucheza soka safi
kwa kufuata maelekezo anayopewa wakati wote,” alisema Mourinho.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *