Habari

JURGEN KLOPP ASEMA NI MAPEMA MNO KUITABIRIA LIVERPOOL UBINGWA

on

HAKUNA ubishi Liverpool wazuri
msimu huu acha kabisa. Wameanza vizuri msimu na wanaendelea kupeta wanavyotaka.
Hata hivyo pamoja na ubora wao
wote huo, bosi Jurgen Klopp amesema ubingwa msimu huu kwa timu yake bado
kabisa.
Ni sawa na kauli ya kukatisha tama,
lakini kwa kocha huyo raia wa Ujerumani anaona Ligi ndio kwanza mbichi na
kuongelea ubingwa wa kikosi chake ni sawa na kupoteza muda wakati huu.
“Reds” ni moja ya timu tatu za
juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, inakusanya pointi 20 ikiwa nyuma ya
Manchester City na Arsenal kwa tofauti ya mabao.
Liverpool tayari imeshacheza na
vigogo kama Arsenal, Tottenham Hotspur, Leicester, Chelsea na Manchester United
katika mechi nane za kwanza msimu huu, lakini Klopp anasema ni mapema sana
kufikiria ubingwa kwa sasa.
“Sijali. Ni masuala ya kawaida
kwenye soka timu inapofanya vizuri watu wanaanza kuzungumzia nafasi ya ubingwa.”
“Sishawishiki kuamini kila
kinachozungumzwa na watu kuhusu sisi. Safari bado ni ndefu na kwa sababu hiyo
huwezi kuzungumzia masuala ya ubingwa kwa sasa,” alisema kocha huyo wakati
akizungumza na waandishi wa habari.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *