KALA JEREMIAH APATA WANANE WA “WANA NDOTO REMIX”

WASANII wanane kati ya zaidi ya 50 waliojitokeza kwa ajili ya kushiriki katika wimbo wa “Wana Ndoto Remix”, wamechaguliwa kushiriki katika wimbo huo unaorendelea kuandaliwa.

Rapa Kala Jeremiah alisema baada ya kutangaza kuwa wanahitajika wasanii wa kushiriki katika wimbo huo walijitokeza wengi kiasi hicho ndipo ukafanyika usaili wakapatikana wanane.

“Maelekezo yalikuwa ni kwamba kila mmoja aandike mashairi kuhusu watoto na changamoto zao na kisha arekodi na kutuletea na ndivyo walivyofanya wote, lakini kwa sababu tulikuwa tunahitaji wanane ikabidi tuchukue idadi hiyo,” alisema.


Alisema, walengwa walikuwa ni wasanii wachanga na kwamba kila mmoja alionyesha uwezo mkubwa na sio kwamba waliochaguliwa walikuwa bora kuliko wengine ila ni kwa sababu ya idadi tu.

No comments