KALA JEREMIAH: SINA MPANGO WA KUTOA ALBAMU MPYA MWAKA HUU

MSANII wa muziki wa Hiphop, Kala Jeremiah amefunguka kwa kusema kuwa mwaka huu hana mpango wa kuachia albamu mpya kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwenye albamu iliyopita.

Akizungumza Kala alisema albamu yake iliyopita bado inaendelea kumpatia shavu hadi sasa.

“Kusema ukweli kazi ambayo niliifanya kwenye albamu yangu iliyopita ilikuwa kubwa sana, albamu yangu ilikuwa na nyimbo 23,” alisema Kala.

“Hata msanii ufanye vipi huwezi kuachia nyimbo 23 ndani ya mwaka mmoja hata miwili, kama ukiachia nyimbo moja moja, kwahiyo mimi najua albamu yangu bado ina muda wa kutosha kwa wananchi mwaka huu, sina mpango wa kuachia albamu,” alisema.


Kala kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa “Wana Ndoto” ambao umetoka miezi miwili iliyopita.

No comments