KIFO CHA SALOME KIWAYA PIGO KWA MUZIKI WA DANSI, UREMBO NA SIASA


TASNIA ya muziki wa dansi imepata pigo kubwa baada ya msanii na mmiliki wa Saki Stars Band ya Dodoma mama Salome Kiwaya (pichani juu) kufariki dunia kwa ajali mbaya ya gari.

Likini si muziki wa dansi pekee bali hata kwa upande wa urembo, kwani Kiwaya ndiye aliyekuwa mwandaaji wa Miss Dodoma na Miss Tanzania Kanda ya Kati.

Salome Kiwaya amefariki Ijumaa jioni kwa ajali iliyohusisha magari matatu ambapo gari aliyokuwepo mmiliki huyo wa Saki Stars aina ya Noah ilivaana vibaya na gari kubwa la mizigo.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Emaus nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Salome Kiwaya ndiye aliyemwibua Emilly Adolf Miss Tanzania wa mwaka 1995.


Kifo cha Salome Kiwaya ni pigo pia kwa upande wa siasa kwani hadi mauti yanamkuta, alikuwa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Dodoma.
Hii ndiyo ajali iliyokatisha uhai wa Salome Kiwaya


No comments