KIM KARDASHIAN AREJEA LOS ANGELES KIMYAKIMYA

STAA Kim Kardashian amenaswa akirejea kimiyakimiya nyumbani kwake jiji Los Angeles ikiwa ni takribani wiki moja tangu aporwe na vibaka mjini Paris, nchini Ufaransa.

Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 25 alinaswa mwishoni mwa wiki wakati akienda kula chakula cha usiku huku amevalia nguo ndefu nyeusi zilizomfunika kichwani na kubakiza sura yake tu.

Vyanzo vya habari viliuambia mtandao wa E newz kwamba mama huyo wa watoto wawili alikuwa ameambatana na mlinzi wake.

“Alikaa muda wa dakika 30 ndani ya mgahawa uliopo Beverly Hills,” kieleleza chanzo cha habari.

“Alikuwa na rafiki yake wa kike na alikuwa akionekana mwenye aibu na hakutaka aonekane,” kiliongeza chanzo hicho cha habari.


Tangu wanaume watano wamvamie hotelini jiji Paris na kisha kumfungia bafuni na kisha wakatoweka na vitu vyemnye thamani yapauni mil 9, Kim amekuwa ni mtu wa kujificha na amewahi kupigwa picha mara moja tu siku hiyo.

No comments