KIM KARDASHIAN AVAMIWA NA WEZI WENYE SILAHA UFARANSA... aporwa vito, mapambo, pesa

ULINZI umeimarishwa katika kila pembe ya jiji la Paris, Ufaransa baada ya wezi wenye silaha kumwibia mwigizaji na mwanamitindo marufu wa Canada anayeishi Marekani, Kim Kardashian.

Ingawaje inafichwa na mamlaka husika kutokana na mambo ya kiusalama, lakini imefichuliwa kuwa mwanamitindo huyo alikuwa amepanga kwenye hoteli ya nyota tano ya Hotel de Pourtales jijini Paris.

Wezi hao walimvizia Kim Kardashian akiwa peke yake hotelini Jumapili iliyopita baada ya walinzi wake kutoka na kumwacha akiwa faragha ili kujipumzisha na kumpora vitu kadhaa vya thamani, zikiwemo mkufu, pete, mapambo mengine pamoja na fedha taslimu alizokuwa nazo.

Polisi wamesambazwa kila kona ya jiji wakiwasaka watu walioshiriki kwenye wizi huo ambao hata hivyo walificha nyuso zao kwa vinyago “mask” ili kutotambuliwa.

Kim Kardashian alikuwa huko kwa ajili ya kuhudhuria maonyesho ya Paris Fashion Week na haijajulikana mumewe Kanye West alikuwa wapi wakati wezi hao walipomvamia.

No comments