KIMBUNGA CHA ARSENAL NI BALAA CHAMPIONS LEAGUE … Ludogorets yalala 6-0 Emirates, Ozil apiga hat-trick


ARSENAL moto chini! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya washika bunduki hao kufanya mauaji Ligi ya Mabingwa kwa kuifumua Ludogorets Razgrad 6-0.

Mesut Ozil amefunga mara tatu dakika ya 56, 83 na 87 huku Alexis Sanchez akiwa ndiye aliyefungua karamu ya magoli dakika ya 12.

Winga asiyeshikika kwa hivi sasa Theo Walcott, aliifungia Arsenal bao la pili dakika ya 42 wakati Alex Oxlade-Chamberlain alipachika bao la tatu dakika ya 46.

No comments