KIUNGO wa klabu ya Rangers ya Scotland, Joey Barton anakabiriwa na adhabu kwa kucheza kamari kinyume na sheria za soka nchini humo.

Barton anatuhumiwa na chama cha soka nchini Scotland kwa kuweka dau mara 44 kati ya Julai 1 na Septemba 15, mwaka huu.

Barton atarejea katika klabu hiyo baada ya kufungiwa kwa wiki tatu kutokana na utovu wa nidhamu.

Chama cha soka nchini humo, SFA kupitia sheria yake kifungu cha 33, inakataza wachezaji, makocha, maofisa wa klabu na waamuzi nchini humo kuweka dau kuhusu matokeo ya michezo popote pale duniani. 


Mwezi Mei, kiungo wa Partick Thistle, Steven Lawless alifungiwa michezo sita baada ya kuthibitika kuwa alicheza kamari ya michezo 513.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac