KIWANGO CHA BAYERN MUNICH CHAMKUNA THOMAS MULLER

STAA Thomas Muller anaonekana kukunwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake ya Bayern Munich usiku wa kuamkia jana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na kuwawezesha kuondoka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya PSV.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Allianz Arena, vijana hao wa kocha Carlo Ancelotti waliingia dimbani wakiwa wameshatoka kapa mara atu mfululizo bila kupata ushindi lakini wakaweza kuzinduka na kuwatembezea kipigo Waholanzi hao.

Alikuwa Muller ambaye alifungulia mvua ya mabao kwa kupachika la kwanza ikiwa ni la tatu msimu huu kabla ya nyota mwenye kiwango cha hali ya juu, Joshua Kimmich kupachika la pili.

Hata hivyo, Luciano Narsiagh aliisawazishia PSV bao moja lakini Roberto Rewandowsk na Arjen Roben wakaongeza mengine mawili baada ya timu hizo kutoka mapumziko.
“Tulianza na kasi tangu dakika ya kwanza,” Muller aliiambia tovuti ya klabu hiyo.

“Tulifanya mashambulizi mengi hususan dakika 30 za kwanza. Ulikuwa ni mchezo mzuri. Tulitaka kuonyesha kiwango kizuri tofauti na ilivyokuwa katika mechi chache zilizopita. Bao la kwanza lilikuwa muhimu kwa sababu tulikuwa tukijutia nafasi tulizozipoteza mwanzo,” aliongeza staa huyo.


Kwa upande wake Robben alisema kuwa anavyodhani Bayern walistahili kushinda lakini alisema kuwa hakuweza kucheza katika ubora wao kwa muda wote wa dakika 90.

No comments