KLOPP ASEMA ANAKUNWA ZAIDI NA DAVID SILVA WA MANCHESTER CITY

MENEJA wa majogoo wa jiji, Liverpool, Jurgen Klopp amemtaja David Silva wa klabu ya Manchester City kama mchezaji pekee katika Ligi Kuu Uingereza anayemvutia kwa kiasi kikubwa. 

Akiongea katika kipindi cha Sky Sport Monday Night Football, Klopp ameweka wazi mapenzi yake kwa mchezai huyo kutokana na aina ya uchezaji wake.

“Nampenda sana David Silva, ni mchezaji wa aina yake. Anazunguuka uwanja mzima, ana akili nyingi akiwa uwanjani pamoja na mtazamo chanya muda wote.”

“Hata kama sijasikia jina lake likitamkwa sana kufuatia mwanzo mzuri wa klabu yake ya Man City kwenye msimu huu wa Ligi ya Uingereza, lakini nina uhakika kabisa kazi yake inaonekana na napenda sana aina yake ya uchezaji.”

“Lakini hata hivyo sivutiwi sana na wachezaji wa timu nyingine kwani wana hatari kubwa pale unapokutana nao,” alisema Klopp.


Klopp ameanza vizuri msimu huu akiwana kikosi cha Liverpool ambacho kimeshinda michezo mine ikiwemo dhidi ya Arsenal na Chelsea ugenini, ametoa sare mara moja na kufungwa mchezo mmoja.

No comments