KLOPP AWAPA NENO LA MATUMAINI MASHABIKI WA LIVERPOOL

MENEJA wa Liverpool Julgen Klopp amekichambua kikosi chake cha msimu huu na kisha kuweka neno la matumaini kwa mashabiki wa majoo hao wa jiji.

Katika mahojiano na Sky Sports Klopp alisema hadi sasa vijana wake wameonyesha dhamira ya kupambana kwa ajili ya kuona wanamaliza katika nafasi nzuri ifikapo mwishoni mwa msimu.

Akinukuliwa kocha huyo wa zamani wa Borrusia Dortmund alisema wachezaji wa msimu huu wanacheza kwa ushinadani ambao wanaifanya timu kuanza vizuri katika Ligi ya Primier msimu huu.

“Vijana wangu wameanza Ligi vizuri, wanacheza kwa ushindani ambao nadhani wanaweza kufanya vyema zaidi.”

“Kila mmoja anapambana kwa ajili ya kuipa timu mafanikio, ninaamini wataendelea kupambana kwa ajili ya kuona wanakuwa washindani baina ya kila timu pinzani,” alisema Klopp.

Liverpool ambao mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa Ligi ilikuwa mwaka 1990, waliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Hull City ambapo awali waliibuka kidedea walipoumana na Arsenal, Chelsea huku wakiwababua mabingwa Leicester City kwa mabao 4-1.


Mechi pekee waliyopoteza ni ile waliyofungwa na Burnley.

No comments