KLOPP: LAZIMA NITARUDI UJERUMANI NITAKAPOSTAAFU UKOCHA

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp ameweka bayana azma yake ya kurudi Ujerumani baada ya kustaafu kufundisha kandanda nchini England.

Klopp amepanga kustaafu kabla ya kufikisha miaka 60.

Ikumbukwe Klopp ana miaka 49 sasa na alianza kuinoa Mainz mwaka 2001 na kuwa na wakati mzuri alipotua Borussia Dortmund kabla hajachukua mikoba ya Brendan Rodgers aliyetimkia Uskochi.

Wachambuzi wa kandanda nchini hapa wanasema Klopp anayafurahia maisha Merseyside lakini hafikirii kama atakaa zaidi ya muongo mmoja.


“Itafika siku ambayo nitaamua kwamba sasa imetosha. Sitaweza kuwa kocha hadi miaka 60. Hakika nitarudi zangu Ujerumani na kuishi huko, lakini sifikirii kama nitarudi huko kama kocha,” alisema Klopp.

No comments