KLOPP SASA KUSAJILI KWA KUWAPANDISHA DARAJA MAKINDA WA KIKOSI CHA PILI LIVERPOOL

BOSI wa majogoo wa jiji la Liverpool, Jurgen Klopp ameanza kuangalia uwezekano wa kuanza kusajili kwa kuwapandisha daraja “Makinda” wa kikosi cha pili cha klabu hiyo.

Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund, amesema kwamba amewatazama wachezaji hao wa kikosi cha pili ameona hawana tofauti na baadhi ya wachezaji ambao watu wanashindania katika soko la wachezaji duniani kwa sasa.

Klopp amesema kwamba akili yake kwa sasa ni kuangalia wachezaji wa kikosi cha pili kabla ya kutumia pesa nyingi zaidi kwa ajili ya kuwapa namba wachezaji kutoka nje ya Liverpool.

Kauli hiyo inawalenga makinda kama Sheyi Ojo, Ryan Kenta, Kevin Stewart na Ovie Ejaria.

“Kila nikiwatazama hawa vijana naona tutatumia bure fedha nyingi kusaka majina makubwa.

Vijana hawa wana uwezo wa hali ya juu na tayari ni kama wameiva kwa kazi ambayo unaweza kuwapa.

“Sina wasiwasi nao, nitawapa kazi katika kikosi cha wakubwa,” amesema.


Amesema nyota ambao anataka kuwapandisha kwenye kikosi cha kwanza ni pamoja na Sheyi Ojo, Camoron  Brannagan, Pedro Chirivella na Kevin Stewart ambao anaamini watakuja kusaidia Liverpool.

No comments