KOCHA AAMINI VARDY, MAHREZ, SLIMANI WANAWEZA KUIFANYA LEICESTER KUTETEA UBINGWA

KOCHA wa Leicester City, Claudio Ranieri anajua kwamba kuna ushindani mkubwa katika Ligi Kuu lakini lazima awasuke upya washambuliaji wake na kutengeneza pacha nzuri zaidi ya Jamier Vardy, Riyad Mahrez na Islam Slimani.

 Ranieri amesema kwamba washambuliaji hao watatu wanaweza kurejesha matumaini ya kuifanya timu kutetea ubingwa wake ingawaje amesema kwamba hali hiyo inaweza kuwa ngumu zaidi.

“Kama unaangalia picha halisi ya Ligi Kuu unaona wazi kwamba msimu huu hatujaanza vizuri. Tumefunngwa katika mechi ambazo tulitakiwa tushinde na hapa ndipo unapoona kwamba kuna ugumu wa kutetea taji,” amesema.

Hata hivyo Ranieri amesema kwamba Mwingereza Vardy na pacha wake uwanjani raia wa Algeria Mahrez na Slimani wako katika ubora wa hali ya juu.

“Kuna uwiano mzuri sana, ninataka kuona wanasimama katika utatu mkubwa ambao unaweza kuibeba timu kuliko wakati mwingine” amesema.


Slimani amesajiliwa kwa uhamisho wa pauni mil 30 kutoka Sporting Lisbon na amekuwa akionyesha kwamba amekuwa mtu muhimu katika kikosi hicho kwa wakati huu.

No comments