Habari

KOCHA ANCELOTTI ASEMA GUARDIOLA AMEMWACHIA KAZI NYEPESI MANCHESTER CITY

on

KOCHA wa Bayern Munich, Carlo
Ancelotti amedai kuwa ameachiwa kazi nyepesi na aliyekuwa kocha wa timu hiyo,
Pep Guardiola ambaye amejiunga na klabu ya Manchester City.
Ancelotti amesema kuwa anaamini
atafanikiwa katika klabu hiyo ya Bayern Munich kutokana na Guardiola kuiwekea
njia ya mafanikio klabu hiyo.
Guardiola akiwa katika klabu
hiyo ya Bayern alifanikiwa kutwaa mataji saba katika misimu mitatu ambayo
aliitumikia ikiwa pamoja na kutwa taji la Bundesliga.
Ancelotti amedai kuwa anavutiwa
na uezo wa wachezaji hao ambao umeachwa na kocha Guardiola.
“Ni kazi nyepesi sana kwa sasa
katika klabu hii kwa kuwa nimewakuta wachezaji wakiwa katika ubora wa hali ya
juu.”
“Ninaamini ubora wa timu hii
umeachwa na Guardiola, nimeikuta timu ikiwa katika ubora wa hali ya juu hivyo
sina kazi kubwa ya kuifundisha.”
“Misingi ambayo imeachwa na
Guardiola ninaamini siwezi kuiacha au kuibadilisha kwa sasa kwa kuwa mizuri na
itanipa mafanikio, japokuwa nina mipango yangu ambayo ninaweza kuiweka hapa,”
alisema Ancelotti.
Bayern Munich kwa sasa inashika
nafasi ya kwanza katika msimu wa Ligi ikiwa na pointi 16 huku nafasi ya pili
ikichukuliwa na Hertha Berlin ambayo ina pointi 13 baada ya timu hizo kucheza
michezo sita.
“Ninajua kwamba timu yangu
inafanya vizuri. Nimekuwa nikiiangalia timu hii kwa misimu mitatu iliyopita,
hivyo kikubwa ni kuendelea na kasi hii kwa ajili ya kuipa mataji,” aliongeza.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka
57 aliwahi kuzifundisha klabu kubwa duniani kama vile AC Milan, Paris
Saint-Germain, Real Madrid pamoja na Chelsea.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *