KOCHA ARGENTINA ASHANGAZWA NA LONEL MESSI KULIFAHAMU SOKA

KOCHA wa timu ya Taifa Argentina, Edgardo Bauza ameshangazwa na jinsi straika Lionel Messi anavyolifahamu soka na akasema kuwa anafahamu kila kitu kuhusu mchezaji huyo.

Kwa sasa Messi yupo nje ya uwanja akisumbuliwa na nyonga lakini anashukuru mafanikio aliyoyapata akiwa na Barcelona.

Hata hivyo Bauza ambaye alizungumza na Messi kabla ya kuamua kurejea katika kikosi cha timu ya taifa, alisema kwamba anashangazwa na jinsi straika huyo alivyo.

“Kinachonishangaza mimi ni jinsi anavyofahamu soka kwa sababu anafahamu kila kitu kuhusu soka, wachezaji wenzake, ufundi wa timu kwa ujumla anafahamu kila kitu,” kocha huyo aliuambia mtandao Sport.


“Mara zote huwa namzimia mchezaji ambaye anafahamu vitu vingi katika soka lakini kwa huyo ananishangaza zaidi,” aliongeza kocha huyo.

No comments