KOCHA FRANK DE BOER AWAJIA JUU WACHEZAJI WAKE KWA KURIDHIA MABAO 2-1 DHIDI YA CAGLIARI

KOCHA wa Inter Milan, Fank De Boer amewacharukia wachezaji wake baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Cagliari.

Mbali ya kuwa nyumbani kwenye uwanja wa Sansiro, kilichomkera zaidi kocha huyo raia wa Uholanzi ni kitendo cha timu yake kupoteza mchezo huo licha ya kuwa mbele kwa matokeo ya bao 1-0.

Inter walipata bao la kuongoza kupitia kwa Joao Mario lakini mabao ya Federco Meichiorri na SDamir Handanovic yaliiwezesha Cagliari kuzoa pointi zote tatu katika mmchezo huo wa Seria A.


“Tulicheza vizuri kipindi cha lkwanza ingawa tungeweza kufanya vizuri zaidi kama tungetumia nafasi za ndani ya boksi," alisema kocha huyo.

No comments