KOCHA nguli katika Ligi Kuu ya England, Harry Redknapp aliyezinoa timu tano kwa nyakati tofauti, amefichua kuwa kuna upangaji matokeo mkubwa katika Ligi hiyo.

Alisema, anafahamu kuwa kuna nyakati wachezaji wake walipanga matokeo katika mechi walizocheza.

Kwa nyakati tofauti, Redknapp alipata kuzinoa Westham United, Portsmouth, Southampton, Tottenham na Queens Park Rangers.

Mbali na Redknapp, pia mmoja wa viongozi wa soka Italia, Pino Pagliara alikiri kufahamu uwepo wa upangaji matokeo katika Ligi Kuu England.


Kocha huyo mkongwe alisema jukumu la kufanya uchunguzi huo halipaswi kuachwa kwa FA pekee bali bodi ya FIFA ya kupambana na rushwa michezoni.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac