KOCHA RANIERI ASISITIZA KUENDELEA KUMFUKUZIA ADRIEN SILVA WA SPORTINGLISBON

KOCHA wa Leicester City, Claudio Ranieri amesema kwamba anaendelea kumfukuzia nyota wa Sporting Lisbon ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho, Adrien Silva.

Kumekuwa na habari zinazoendelea kusambaa kwamba klabu bingwa hiyo ya Uingereza itakuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili nyota huyo katika uhamisho wa dirisha dogo la mwezi Januari.

Ranieri amesema kwamba anataka kuhakikisha anamchukua nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 na bei yake imetajwa kwamba inaweza kuwa pauni mil 21.

Hata hivyo kocha huyo amesema kuwa wanaweza kukaa upya na klabu hiyo ya Ureno kama ofa hiyo haitoshi, lakini nia yake ni kumnyaka nyota huyo kwa gharama yoyote.

“Tunaendelea kutafuta wachezaji wengi wa maana sana na kwakweli lazima niseme kwamba mmoja wa wachezaji ambao tunawafukuzia sana ni pamoja na Adrien Silva ambaye ni mchezaji mzuri sana,” amesema Ranieri.

“Kuna haja ya kuimarisha sana kikosi hiki. Tunaweza kuimarisha idara zote kwa nia ya kutetea ubingwa wetu ingawaje sio jambo la uhakika sanakwamba lazima tuwe mabingwa,” ameongeza.


Kocha huyo amesema kwamba baada ya kipigo kutoka kwa Manchester United wiki iliyopita, kuna kitu kikubwa anaweza kuwa amejifunza na anakifanyia kazi.

No comments