Habari

KOCHA UFARANSA AKIRI POGB ALICHEMSHA MECHI DHIDI YA BULGARIA… amtaka kuboresha kiwango chake

on

KOCHA wa timu ya taifa Ufaransa, Didier Deschamps ameafiki kuwa kiungo wake, Paul Pogba alichemsha kwenye mechi
ya ushindi ya Bulgaria mwishoni mwa wiki iliyopita na kumtaka kuboresha kiwango
chake.
Les Blues walipata ushindi wa
kwanza kwenye mechi hiyo ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018, shukrani kwa mabao mawili kutoka kwa Kevin Gameiro, Dimitri Payet na Antoine
Griezmann.
Pogba alikuwa muhimili katika
nafasi ya kiungo kwenye michuano kwenye Euro 2016 lakini juzi alichemsha.
“Anaweza kufanya vizuri zaidi
na lazima abadilike,” alisema Deschampis.
“Anapokuwa na majukumu ya
kuingo mkabaji na akacheza vile, hicho siyo kiwango chake.

“Ana kila sababu ya kufanya
vizuri anasifa ambazo wengine hawana.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *