KOCHA WA AC MILAN AMPONDA CESC FABREGAS... asema hawezi kuwa mbadala wa majeruhi Riccardo Montolivo

KOCHA wa timu ya AC Milan, Vincenzo Montella ni kama akamponda kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas baada ya kusema kuwa mchezaji huyo sio mbadala wa kumrithi nyota wake majeruhi, Riccardo Montolivo.

Kwa sasa Montolivo anakabiiwa na kipindi kirefu cha kukaa nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti na kumekuwepo na tetesi mjini Milan zikidai kuwa Fabregas atakwenda kuziba pengo lake.

Hata ivyo, pamoja na vinara hao wa Ligi ya serie A kuhusishwa na staa huyo raia wa Hispania, lakini jana Montella hana mawazo ya kumsajili Febregas.

“Tunahitaji mchezaji mwenye uwezo kama wa Montolivo, mmoja wa wanaofahamu jinsi ya kucheza viungo viwili. Fabregas hana uezo huo,” Montella aliuambia mtandao wa Corriere della serra.

“Nadhani nafasi ya Montolivo haitazibika mapema, ni mchezaji muhimu uwanjani na kenye vyumba vya kubadilisha jezi na kukkosa ni pigo kubwa mno tofauti na watu wanavyodhania,” aliongeza kocha huyo.

No comments