KOSCIELNY ASEMA HAFAHAMU KAMA ALIUNAWA MPIRA MECHI YAO DHIDI YA BURNLEY

STAA wa Arsenal, Laurent Koscielny amesema kwamba wala hafahamu kama aliushika mpira wakati akiwa kwenye harakati za kufunga bao wakati wa mchezo ambao walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Burnley zikiwa ni dakika za mwisho za mchezo huo wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo huo Burnley wakiwa kwenye uwanja wao wa Turf Moor walionokana kucheza vizuri na kuonekana kama wangeweza kuondoka angalau na pointi kabla ya Koscielny kuukwamisha mpira kimiani katika muda wa nyongeza za kipindi cha pili.

“Sifahamu kama niliunawa mpira. Nilijaribu kwa mguu wangu wa kushoto na sifahamu kama uligusa kwenye mkono wangu ,” alisema nyota huyo.


“Mwamuzi ndiyo aliyekubali bao na hivyo unachotakiwa ni kuheshimu uamuzi wake,”aliongeza staa huyo.

No comments