KR MULLER APOTEZEA KAULI YA JUMA NATURE KUWA ANAKULA "UNGA"

MSANII maarufu wa Bongofleva KR Muller amesema hawezi kuzungumzia kauli ya Juma Nature ya kumhusisha yeye KR na utumiaji wa dawa za kulevya kwavile hayuko nae karibu.

KR alisema hayo alipohojiwa na ITV na kutakiwa kutoa kauli yake kuhusu tuhuma ambazo Nature amekuwa akizitoa mara kwa mara kwamba anatumia dawa za kulevya.

“Tuzungumzie mambo mengine lakini mimi sitaki kumzungumzia Juma Nature kwa kuwa hayuko hapa, mimi napenda nikimzungumzia mtu na yeye awepo,” alisema KR. 


Msanii huyo aliwatoa hofu mashabiki wake kwamba picha zilizotapaka akionekana amelala kwenye maeneo yasiyofaa alikuwa amechoka kutokana na kazi anazofanya.

No comments