KUDADADEKI… CRISTIAMNO RONALDO ATUPIA “HAT-TRICK” YA 43

IMANI za Zinedine Zidane kwa Cristiano Ronaldo zimezaa matunda pale straika huyo Mreno alipofgunga Hat-trick katika ushindi wa Real Madrid wa mabao 4-1 dhidi ya Alaves juzi.

Kocha huyo wa Madrid alimtetea Ronaldo akisema “Ni kinara wa wazi” wa mbio za Ballon d’Or wiki hii licha ya ukame wa mabao katika mechi tano za Ligi.

Ronaldo ambaye alipumzishwa katika mechi ya Kombe la Mfalme ambayo Madrid walishinda 7-1 dhidi ya Cultural Leonesa jumatano iliyopita pasmoja na kufunga “hat-trick” juzi alikosa na penati.


Ilikuwa ni “hat - trick” ya 43 ya Ronaldo katika maisha yake ya soka ya 31 akizifunga katika mechi 243 alizocheza kwenye La Liga huku pia akifikisha jumla ya magoli 350 katika Ligi tangu akiwa Sporting Lisbon, Man united na Real.

No comments