KUMBE KOCHA ANTONIO CONTE ALIYATARAJIA MATOKEO MABOVU KWENYE TIMU YAKE

BOSI wa Chelsea, Antonio Conte amezungumzia udhaifu wa klabu yake Ligi Kuu England baada ya kipigo cha hivi karibuni cha bao 3-0 kutoka Arsenal. 

Kipigo hicho kilikamilisha safari ya kucheza mechi tatu bila ushindi.

Kabla, Blues walinyukwa mabao 2-1 na Liverpool kwenye uwanja wa Stamford Bridga wakitangulia pia kupoteza pointi baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Swansea City pamoja na kuongoza kwa bao la mapema.

“Sishangazwi na matokeo hayo kwasababu unapobadili wachezaji ina maana kuna tatizo kwenye timu yako,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mchezo dhidi ya hull City juzi.


“Unapokuja sehemu mpya kwanza lazima utatue tatizo lililopo kisha uanze kuizoea hali. Wakati mwingine inaweza kuwa rahisi kumaliza tatizo mapema na wakati mwingine unahitaji muda mwingi,” alisema Conte.

No comments