Habari

LEYLA RASHID, ISHA MASHAUZI WAKATA MZIZI WA FITINA DARLIVE

on

HATIMAYE ule mzizi wa fitina
kuhusiana na tambo za nani mkali kati ya Isha Mashauzi na Leyla Rashid umekatwa
usiku wa jana kuamkia leo, ndani ya Darlive, Mbagala, Dar es Salaam.
Katika pambano kali lililowakutanisha
mastaa wawili hao, mashabiki walionekana kujigawa kila upande na kufanya kwa
kuwashangilia wote kwa nguvu na kufanya kuonekana kama waliogawana pointi.
Isha ndie aliyekuwa wa kwanza
kutumbuiza, kufuatia kura iliyomdondokea baada ya kurushwa kwa ‘shilingi’ mara
zilipomaliza kutumbuiza bendi za Mashauzi Classic na Jahazi zilizokuwa
zikisindikiza pambano hilo.
Kete zake mbili za “Mapenzi
Hayana Dhamana” na “Kismeti” ziliulipua ukumbi kwa kelele za vifijo, kabla hajampisha
Leyla aliyeingia na vibao “Langu Rohoni” na “Kwa Hilo Hujanikomoa” ambaye nae alipokelewa kwa
shamrashamra za hali ya juu.
Awamu ya pili nayo ilikuwa ya
kishindo kwa kila mmoja ambapo Isha aliibuka na “Sura Surambi” na “Nimpe Nani”
wakati Leyla alikuja kufunga dimba kwa vibao “Sina Muda Huo” na “Nina Moyo Sio
Jiwe”.
Washereheshaji Aisha Mbegu “Sauti ya Ninga” na
Mwasiti Robert “MC Mabobish” nao walionekana kuliongezea ladha pambano hilo kwa namna
walivyojawa na vituko na vibweka, zikiwemo “suprise” za hapa na
pale.
PATA PICHA 20 ZA NAMNA SHOO ILIVYOKWENDA
Ma MC Mwasiti Robert (kushoto) na Aisha Mbegu wakiwakaribisha wawakilishi wa Isha Mashauzi na Leyla Rashid kupanda jukwaani kurusha shilingi.

 Hapa mwakilishi wa Isha, Hamadi Mmanga (kushoto) akipeana mkono na mwakilishi wa Leyla, Hemed Hemelaa kabla ya kurushwa kwa shilingi
 Shilingi ikiandaliwa kurushwa 
 Isha akianza kutumbuiza baada ya kura kumdondokea
 Hapa mnazi wa Mashauzi Classic, Mamu Original Mariam akicheza sambamba na Isha
 Isha akiimba kwa hisia
Mwimbaji wa Jahazi Modern, Mohammed Chipolopolo akimtuza Isha
MC Mabobish akimwita Leyla jukwaani baada ya zamu yake kufika
 Isha akimpokea Leyla kwa furaha kuja jukwani
 Wanateta kidogo
 Mazungumzo yanaendelea
 Leyla akiwa ameanza kutumbuiza 
 Hapa mpasho umekolea jukwaani
 “Sauti ya Ninga” sasa imeshindwa kujizuia na kumpandia Leyla jukwaani ili “kujiselfie” nae
 Leyla akimuunga mkono Isha jukwaani kuonyesha kuukubali uwezo wake
 Isha nae hapa amejitosa kumtuza mpinzani wake alipoingia kutumbuiza kwa awamu ya pili
 Isha amekolea… anaamua kusebeneka nae kidogo
 Leyla anakula noti za Isha “aliyelewa” utamu wa kibao”Langu Rohoni” 
Sauti ya Ninga anatangaza kufunga rasmi pambano

Na hivi ndivyo ukumbi wa Darlive ulivyotapika mashabiki waliokuwa na mzuka mwanzo mwisho

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *