LIL WAYNE ASEMA DRAKE ALIWAHI KUTOKA KIMAPENZI NA MSICHANA WAKE WAKATI AKIWA GEREZANI

IMEFICHUKA kuwa kuna kipindi rapa Drake aliwahi kutoka kimapenzi na msichana aliyekuwa mchumba wa mlaki Lil Wayne.

Hayo yamesemwa na Wayne katika jarida lake jipya linaloelezea maisha yake ya gerezani kuanzia mwaka 2010.

Kipindi hicho, wayne alihukumiwa kifungo cha miaka nane gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Katika jarida hilo, Wayne ameelezea mambo mbalimbali yanayomhusu zikiwemo kashfa mbalimbali alizowahi kukumbana nazo zikiwemo kujihusisha na dawa za kulevya.

Hata hivyo staa huyo wa Hiphop hakuweka wazi jina la msichana huyo ambaye alichepuka na Drake, ingawa hakuwahi kuwafumania laivu wawili hao.

No comments