Habari

LIVERPOOL YATHIBITISHA KUENDELEA KUMFUKUZIA ANDREA RANOCCHIA

on

KLABU ya Liverpool
imethibitisha kuwa mpango wao wa kumwania beki Andrea Ranocchia unaendelea kufanywa chinichini
ila kwa uhakika mkubwa.
Taarifa za ndani ya klabu hiyo
zinasema kuwa uongozi wa Liverpool uko katika mchakato wa kumchukua beki huyo
kisiki wa Inter Milan kwa ajili ya kukiimarisha kikosi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Talk
Sport wa Calciomercato, Koch wa Liverpool, Jurgen Klopp amekuwa akivutiwa
sana na beki huyo wa kati wa Inter Milan na wako tayari kumnyakua kwa mkopo.
Ranocchia hajang’ara sana katika kikosi cha kocha Frank de Boer na amekuwa akihusishwa na mipango ya kuondoka katika timu hiyo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, yeye mwenyewe amekuwa akisema kwamba baada ya kushindwa kung’ara akiwa na kocha wake huyo ni vyema akatazama maisha mengine mahali kwingine.

Beki huyo anatajwa kwamba anaweza sasa kuwa na nafasi ya kuhamia Uingereza katika klabu hiyo, sio tu kwakuwa anatafuta changamoto, lakini pia kwasababu Liverpool imekuwa ikihitaji beki wa aina yake. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *