LUKA MODRIC ATAMANI KUMALIZIA SOKA LAKE REAL MADRID

STAA Luca Modric anatamani kuona akimalizia maisha yake ya soka katika klabu ya Real Madrid.

Kiungo huyo raia wa Croatia alipewa mkataba mpya na wababe hao wa jijini Madrid na sasa atabaki klabuni hapo hadi mwaka 2020.


“Nafikiri haitokuwa matra yangu ya mwisho kuongeza mkataba. Ndoto yangu ni kumalizia soka hapa Madrid,” alisema Modric kuwaambia waandishi wa habari.

No comments